SHEIKH PONDA AJISALIMISHA CENTRAL POLISI
Sheikh Issa Ponda |
Katibu mkuu wa
baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda
amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central.
Kiongozi huyo wa dini aliwasili leo katika
kituo hicho cha polisi akiwa na wakili wake Abdallah Safari ambapo ni kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa kanda
maalum ya Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.
Kamanda Mambosasa siku ya jana alimwagiza
Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na
matamshi ya uchochezi aliyotoa.
Kwa mjibu wa kamanda huyo,Sheikh Ponda alifanya
makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na
alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo atakamatwa.
Comments