SERIKALI KUANZA KUWASHGHULIKIA WANAOVAA NUSU UCHI
Waziri
wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara
imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao
wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.
Waziri Harison Mwakyembe |
Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala
hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa
wakiwagusa huwajia juu na kulalamika.
Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika
kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo
zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na
zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments