WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KATAVI WATAKIWA KUEPUKA MAZINGIRA YA UKATIRI
Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANAFUNZI wa Shule za Msingi na
Sekondari Mkoani Katavi wametakiwa kuepuka
mazingira yanayopelekea vitendo ya
ukatili na unyanyasaji na kuzingatia
masomo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa
Kitengo cha dawati la jinsia na
watoto katika Jeshi la Polisi Mkoani Katavi SP Zabroni
Ibeganisa katika Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Vitendo vya ukatili na
unyanyasji wa kijinsia iliyofanyika Shule ya Msingi Kawanzige Manispaa ya
Mpanda.
Wanafunzi wa Shule ya ,Msingi Kawanzige |
Aidha SP Ibeganisa amewataka
wanafunzi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa walimu,
viongozi wa serikali na dawati la jinsia na watoto kituo cha polisi.
Kauli mbiu ya Kampeni hii mwaka huu ni Funguka chukua hatua linda mtoto apate elimu.
Comments