WAKALA WA VIPIMO TANZANIA KUZINDUA MATUMIZI YA VIPIMO KESHO MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wakala wa vipimo Tanzania Kesho wanatarajia
kuzindua na kukopesha mizani kwa wafanyabiashara wadogo Mkoani Katavi kwa ajili
ya kuondokana na hasara zinazotokana na kuuza bidhaa mbalimbali pasipo kutumia
vipimo halali.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa wakala
wa vipimo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi Bw.Amos Nzaga katika semina elekezi
kwa wafanyabiashara ambayo imefanyika jana
katika Soko la Buzogwe Manispaa ya Mpanda.
Kwa upande wake Bi.Irene John ambaye
ni Kaimu meneja wa semina ya elimu na mawasilano kutoka makao makuu ya Wakala wa Vipimo Jijini Dar es
Salaam,amesema Mkoa wa Katavi umepewa kipaumbele namba moja,kutokana na
uzalishaji wa mazao ya biashara kwa wingi.
Nao baadhi ya wafanyabiashara katika
semina hiyo,wamesema wanategemea kusaidiwa katika utatuzi wa changampoto
zinazowakabili katika shugfhuli za kibiashara.
Comments