WAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WAMELALAMIKA KUNYANG’ANYWA GARI LA WAGONJWA,HALMASHAURI YATOA UFAFANUZI
Na.Issack
Gerald
Wakazi wa
kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa madai kuwa halmashauri hiyo
imewanyanga’anya gari la wagonjwa ambalo limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa
katika kata hiyo.
Wamesema kuwa wamenyang’anywa gari kwa
madai kuwa wakazi wa Katumba hawana dereva wa kuendesha gari hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri
hiyo Mh.Raphael Kalinga amekanusaha kuwanyang’anya gari la wagonjwa wakazi wa
Kata ya Katumba ambapo amesema lipo kwenye matengenezo baada ya kuharibika.
Aidha Kalinga amesema suala la
kuharibika kwa gari hilo limekwishatolewa ufafanuzi kuanzia kwa viongozi wa
Halmashauri,Mkoa hadi ngazi ya wizara.
Kata ya Katumba ina vijiji 16 na zaidi
ya wakazi elfu hamsini wanaotegemea huduma ya gari hilo.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments