SPIKA AAGIZA MWANDISHI NA WAHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA WAHOJIWE KWA KULIDHALILISHA BUNGE
Kamati ya Maadili,Haki na Madaraka
ya Bunge,inatarajia kuwahoji mwanahabari Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti
la kila wiki la Raia Mwema kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha
bunge,Aprili 9 wiki hii.
Hayo yameelezwa leo Aprili 12
bungeni na Spika wa Bunge,Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa
Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.
Hayo yamekuja baada ya mbunge wa
Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji
iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge
linajipendekeza?”haidhalilishi bunge.
Spika Ndugai leo Aprili 12,ameliambia
bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya
bunge.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments