RAIS MAGUFULI ATAKA WATANZANIA WAMUEZI SOKOINE KWA KUIGA MEMA ALIYOYAFANYA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.John Magufuli ametoa rai kwa watanzania kumuenzi Waziri Mkuu wa Zamani hayati
Edward Moringe Sokoine kwa kujenga umoja,kupiga vita rushwa na kuchapa kazi.
Rais ametoa kauli hiyo kupitia
ukurasa wake wa twitter ikiwa leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Edward Moringe Sokoine
aliyefariki dunia Aprili 12,1984 kwa ajali ya gari.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Dakawa
nje Kidogo ya Mji wa Morogoro wakati akitokea Bumgeni Dodoma Kuelekea Jijini
Dar es salaam.
Amesema watanzania wanapoazimisha
siku hii ya kifo chake, watanzania waige mfano wake kwani alikuwa msema kweli,
asiyeogopa,mpiga vita rushwa,ufisadi,unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia
rasilimali za watanzania kuibwa.
Rais amesema kwa upande wake
anamkumbuka kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa la
Tanzania na anasema alipata taarifa za kifo cha Sokoine tarehe 12 Aprili 1984 akiwa Mpwapwa JKT
nikitumikia jeshi katika kikosi cha “Oparesheni Nguvukazi”.
Comments