WANANCHI KATAVI WATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WAMUENZI SOKOINE KWA KUPELEKA HUDUMA MUHIMU ZA JAMII KWA WANANCHI
Wananchi Mkoani Katavi wamewashauri
viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha Wazairi Mkuu
hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za kijamii kwa
wananchi ikiwemo maji.
Wakizungumza na P5TANZANIA kwa
nyakati tofauti kuhusu kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu hayati
Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki 12,1984 wamesema kuna maeneo mengi
mkoani Katavi ambayo bado yanakosa huduma muhimu kama maji huku hata sehemu
zenye zikipata kwa mgao.
IAidha wametaka hata miradi ya maji
iliyoanzishwa enzi za ukoloni ifufuliwe huku wakisema bado kuna hali ngumu ya
kimaisha ambayo serikali inatakiwa iyatatue kama sehemu ya kumuenzi Sokoine.
Aidha wamesema ni kiongozi
aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi
wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978.
Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine
aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka
1980 na Februari 24 mwaka 1983 hadi kifo
chake kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Bungeni Dodoma kuelekea Jijini
Dar es salaam.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments