RAIS AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Aprili 12,2018 amewapandisha vyeo maafisa wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.
Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali
Venance Salvatory Mabeyo,Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe.Rais
Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni
Jenerali.
Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa
Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa
na Luteni Jenerali wawili.
Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry
Kamunde kuwa Meja Jenerali.
Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ
kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni
Kanali na kuwa Kanali.
Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu,J.J Mwaseba, A.S
Mwamy,R.K Kapinda,C.D Katenga,Z.S Kiwenge,M.A Mgambo,A.M Alphonce,A.P Mutta,A.V
Chakila,M.G Mhagama,V.M Kisiri,C.E Msolla na S.M Mzee.
Wengine ni C.J Ndiege,I.M Mhona,R.C Ng’umbi,S.J Mnkande, A.C
Sibuti,M.M Mumanga,I.S Ismail,M.N Mkeremy,G.S Mhidze,M.A Machanga,S.B Gwaya,
P.K Simuli na M.E Gaguti.
Halikadhalika Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Luteni
Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide
de Camp – ADC)
Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi
ya Kanali Mbaraka Naziad Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia
Jenerali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments