ASKOFU NYAISONGA ATAKA WAKRISTO WATENDE MEMA


Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga
Katika maadhimisho ya siku ya Ijumaa kuu kwa wakristo,Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi  Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga amewataka waumini wa kikristo kuendelea kutenda kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungu wa Kwaresma.
Askofu Nyaisonga ametoa wito huo leo katika adhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu katika ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda.
Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji.
Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu.
Sikukuu ya pasaka kwa mwaka 2018 inatarajiwa kuadhimishwa Aprili mosi mwaka huu.
Ijumaa kuu kitaifa imeadhimishwa Mkoani Mbeya.
Habari Zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA