SERIKALI YA WILAYA YA MLELE KWENDA KWA WAZIRI KUPATA UHAKIKA LINI HOSPITALI ITAJENGWA



Na.Issack Gerald-MLELE
SERIKALI ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imesema inatarajia kwenda kumuona Waziri wa Afya ili kupata uhakika lini wananchi waliotoa ardhi yao kujengwa hospitali ya wilaya hiyo watalipwa fidia zao.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Issa Njiku, amewaambia wananchi wa wilaya hiyo wawe wavumilivu kwani baada ya muda mfupi watapewa majibu ambayo yatamaliza tatizo la muda mrefu la kudai fedha zao za fidia.
Amesema wananchi wamekuwa wakidai fedha zao ili wanunue ardhi katika maeneo mengine na kuendelea na shughuli za uzalishaji ikiwamo kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba bora na  za kisasa.
Mmoja wa wananchi wanaodai fidia, Francis Mikidadi, amesema kuwa wamechoka kuvumilia na hawaamini kuwa viongozi wao wanalifuatilia suala lao kwa umakini kwani lingekuwa limekwisha malizika.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA