RAIS MAGUFULI ATOA AHGIZO LA KIUCHUMI KWA BOT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni katika biashara na huduma
hapa nchini ili kulinda nguvu ya fedha ya Tanzania na kukabiliana na uhalifu wa
kifedha.
Mhe.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akifungua tawi la benki
ya CRDB-LAPF Dodoma na kubainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha uchumi
wa nchi.
Aidha,Mhe.Rais
Magufuli ameitaka BOT kuongeza usimamizi wa benki zinazoendesha shughuli zake
hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinajiunga na mfumo wa ukusanyaji
mapato kwa njia ya kielektroniki na kufuatilia kwa ukaribu utendaji wake wa
kila siku ili ziwe na manufaa kwa nchi.
Wakati huo huo Mhe.Rais
Magufuli ameipongeza benki ya CRDB kwa kuendeshwa kwa ufanisi tangu
ilipobinafsishwa kutoka Serikalini ambapo katika kipindi cha miaka 10 imelipa
kodi serikalini kiasi cha Shilingi Bilioni 800,imetoa ajira kwa Watanzania
3,200,imetoa gawio Serikalini la Shilingi Bilioni 19.5 mwaka huu na imetoa
mikopo yenye thamani ya Shilingi Trilioni 3.5 ambapo Shilingi Trilioni 1 kati
yake zimeelekezwa katika sekta ya viwanda na kilimo.
Rais Magufuli
akizungumzia kuhusu kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi
Mhe.Rais Magufuli amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali zitakazoongeza
kasi hiyo zikiwemo kupunguza kiwango cha kisheria cha sehemu ya amana za benki
za biashara kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu kutoka asilimi 10 hadi 8,kushusha
riba ya Benki Kuu mara mbili kutoka asilimia 16 hadi 9,kutoa mikopo maalum kwa
benki za biashara,pamoja na Benki Kuu kununua fedha za kigeni kwenye soko la
jumla la benki ili kuongeza ukwasi wa shilingi kwenye uchumi.
Mhe.Rais
Magufuli ametoa wito kwa benki zote nchini kuanzisha matawi ya benki vijijini
na kuwakopesha wajasiriamali ili waongeze uzalishaji hasa kilimo na viwanda na
pia ametaka wananchi wanaopata mikopo wazingatie kurejesha.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt.Charles Kimei amempongeza
Mhe.Rais Magufuli kwa juhudi kubwa za kuimarisha uchumi zikiwemo ujenzi wa
viwanda,ununuzi wa ndege,ujenzi wa reli ya kisasa (SGR),ujenzi wa barabara za juu (Flyover) ambapo ameahidi kuwa CRDB yenye
matawi 469 na wateja 3,500,000 ikiwa ndio benki inayoongoza kwa mtandao mkubwa
nchini,itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali na
uwekezaji katika viwanda na kilimo.
Dkt. Charles
Kimei na Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bw. Ally Laay wamekabidhi hundi ya Shilingi
Milioni 100 kwa Mhe.Rais Magufuli kwa ajili ya kuchangia huduma za kijamii na
Mhe.Rais Magufuli amekabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith
Satano Mahenge kwa ajili ya ujenzi wa wodi katika hospitali ya Mkoa Dodoma.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments