WANAWAKE WAJAWAZITO WILAYANI MPANDA WANALAZIMIKA KUBEBA MAJI KUTOKA NYUMBANI MPAKA ZAHANATI KWA AJILI YA USAFI WAKATI WA KUJIFUNGUA
Na.Issack Gerald
Wanawake wote wajawazito katika kijiji cha
Mtambo kata ya Katumba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,
wanalazimika kubeba maji kutoka nyumbani na kuyapeleka katika zahanati ya
Mtambo iliyopo kijijini hapo ili yatumike wakati wakijifungua.
Mganga mfawidhi wa zahanti hiyo Dkt.Daud
Mashama amesema wanawake wajawazito wasipokuja na maji hulazimika
kufuata maji mto Kalutonya uliopo umbali wa kilomita 8 kutoka zahanati ya
Mtambo.
Kaimu
afisa Mtendaji wa kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine amekiri kuwepo kwa tatizo la
maji katika kijiji cha Mtambo huku akisema mara kwa mara kila wanapochimba
visima upatikanaji wa maji umekuwa mgumu.
Kwa upande
wake Katibu wa kijiji cha Mtambo Bw.Fenias Fulujensi pamoja na mambo mengine
amesema wanasubiri uwekaji wa mitambo katika kisima kilichochimbwa ili kusukuma
maji.
Kwa mjibu
wa wakazi wa kijiji cha Mtambo,zahanati ya Mtambo ilijengwa miaka ya 1992
ambapo hata hivyo Juhudi za kutafuta uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo
kuhusiana na tatizo hilo zinaendelea.
Hivi karibuni
wakazi wa Kata ya Katumba walilalamika kukosa maji ya chanzo cha maji ya
Ikorongo wakisema maji kusafirishwa kutoka kata ya Katumba mpaka Mpanda Mjini
na wao kukosa huduma hiyo licha ya chanzo hicho kuwa katika kata yao serikali
haiwatendei haki.
Serikali
ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John pombe Magufuli inajinasibu kuwa
moja kati ya mipango iliyopo katika ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 inasema
inalenga kumtua mama ndoo kichwani ambapo kwa mjibu wa hali iliyopo katika kata
ya Katumba bado ndoo inamlemea mama kichwani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments