MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MUMEWE,WANAWAKE WALAANI
Wanawake wa Mtaa wa Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamelaani vikali kitendo cha Abdalla Ibrahim
Mkazi wa mtaa huo kumtelekeza mkewe Rosemary Robert Ismail mpaka kusababisha
kifo chake kwa kutompatia huduma baada ya kuugua kwa muad mrefu.
Wanawake hao wamesema kitendo ambacho
amekifanya Bw.Ibrahimu ambaye ni mlinzi wa kampuni moja mjini Mpanda ni ukatiri
wa hali ya juu.
Kwa upande wake Muuguzi wa wagonjwa
Majumbani Hadija Mwishehe mkazi wa mtaa wa Mpanda Hotel amesema, alimpatia
huduma ya kwanza mwanamke huyo akiwa nyumbani kabla ya kufariki juzi akiwa
Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo Bw.Abdalla Ibrahim ambaye
ni mume wa Rosemary Robert Ismail amekana kumtelekeza na kumnyima huduma huku
akisema kuwa ameishi naye kwa muda wa wiki moja.
Kwa mjibu wa Bw.Benson Soyi ambaye ni
jamaa wa karibu na marehemu,mpaka sasa ndugu wanaosemekana kuwa wapo Sumbawanga
Rukwa hawajapatikana na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Manispaa ya
Mpanda.
Naye Tekra Pius Kabedi
ambaye ni Mjumbe wa serikali ya Mtaa Mpanda Hotel amethibitisha kupokea taarifa
za kifo hicho mtaani kwake ambapo amesema sababu kubwa ni kukosa kupewa huduma
ya matibabu na chakula.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments