WADAU WA ELIMU WACHANGIA ZAIDI SHILINGI MIL.152 KWA AJILI YA SEKTA YA ELIMU
Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimechangwa na wadau wa
elimu wilayani Tanganyika mkoani Katavi,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya
elimu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael
Muhaga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda
Mjini,ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta
maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Salehe Muhando pamoja na mambo mengine amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Salehe Muhando pamoja na mambo mengine amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Suleima
Kakoso baada ya kuchangia komputa kwa shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na
fedha taslimu,amezishauri halmashauri Mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa
maendeleo walioko ndani na nje ya halmashauri zao ili washiriki kuleta
maendeleo.
Miongoni mwa mafanikio ya harambee
hiyo ni pamoja na Komputa 24 Zenye thamani ya shilingi milioni 48,mifuko ya
simenti 2281 ya Shilingi milioin 41,058,000,vitanda 25 vya aina ya dabodeka vyenye
thamani ya shilingi 5,000,000,Malumalu boksi 200 za shilingi 5,000,000,Bando 1530
za bati zenye thamani ya shilingi 30,400,000.
Vitu vingine ni Fedha taslimu shilingi
400,000,Fedha ahadi Shilingi 17,400,000,Kokoto kubwa Tan 14 za Shilingi 520,000
na Kokoto Vumbi tan 14 za Shilingi 160,000
Wadau wa elimu ambao wameshiriki wanatoka taasisi za
kifedha,wafanyabiashara,madiwani halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara
wilayani Tanganyika,wakulima, pamoja na watu binafsi na idadi yao inakadiriwa
kuwa zaidi ya 200.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments