WALEMAVU WASIOONA 127 WAKIWEMO WANAFUNZI 58 MKOANI KATAVI BADO WANA MATATIZO MAKUBWA YA KUKOSA HUDUMA STAHIKI KATIKA ELIMU NA AFYA
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi
CHAMA cha Wasioona Tanzania TLB
Mkoani Katavi,kimesema Walemavu zaidi ya 127 wasioona waliopo Mkoani
Katavi,bado wanakabiliwa na hatari ya kukosa huduma muhimu mbalimbali kama
elimu,afya na mengineyo muhimu kutokana na jamii kuendelea kuwa na mtazamo
kuwa,walemavu hawana mchango wa kuleta maendeleo.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Tulia Akson akihutubia siku ya fimbo nyeupe Mkoani Mbeya akiwa ndiye Mgeni rasmi(PICHA NA.Issack Gerald) |
Bw.Emmanuel Simon katibu wa TLB taifa akiwasilisha taarifa wakati wa maadhimisho ya siku ya wasioona maarufu siku ya fimbo nyeupe Mkoani Mbeya(PICHA NA.Issack Gerald) |
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
chama cha TLB(Tanzania league of Blind) na Shirikisho la vyama vya watu wenye
ulemavu(SHIVYAWATA) mkoani Katavi Bw.Issack Lucas Mlela,wakati akizungumzia
kilichojili katika maadhimisho ya siku ya wasioona maarufu ‘’siku ya fimbo
nyeupe ‘’ kitaifa yaliyofanyika wiki iliyopita Mkoani Mbeya.
Bw.Mlela amesema,kwa mjibu wa sensa
ya mwaka 2013,jumla ya walemavu wasioona 127 mkoani Katavi walibainika, ambapo
kati ya hao kuna wanafunzi 58 wasioona wanaotakiwa kupatiwa elimu ya uhakika
kama watoto wasio na walemavu.
Aidha Bw.Mlela amesema,taarifa iliyosomwa kwa mgeni rasmi na Katibu mkuu wa TLB taifa Tanzania bara Bw.Emmanuel Simon,iliabainisha kuwa walemavu bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa vyuo vinavyowawezesha kupata ujuzi,ambapo vyuo 2 vya mafunzo vya Rwanzari kilichopo mkoani Tabora na Mtapika kilichopo Wilayani Masasi vilivyokuwa vikitoa ujuzi wa kilimo na useremala vilifungwa na sababu ikiwa ni kukosekana kwa fedha za kuendeleza vyuo hivyo licha ya kuwa walemavu wanaohitaji kusoma wapo wengi.

Changamoto nyingine ambazo zinatakiwa
zipatiwe ufumbuzi ni ukosefu wa miradi ya maendeleo ili kuendeleza maisha ya
kila siku.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Tulia Akson pamoja na mambo mengine alisema,hatua za haraka zimechukuliwa ikiwemo kuunda idara ili kushughulikia vyuo vilivyofungwa ili mwaka wa masomo 2017 walemavu wapate haki ya elimu kama kawaida katika vyuo hivyo.
Aidha Mh.Akson alisema kuwa mahitaji mengine ambayo yalibainishwa katika risala,ataziwalisha katika wizara ili zipatiwe ufumbuzi.
Mwaka huu 2016,kilele cha maadhimisho hayo kilifanyika Oktoba 6 Mkoani Mbeya yakitanguliwa na maandamano yaliyoanza Oktoba 2 na kongamano la Oktoba 5 huku kauli mbiyu ikisema kuwa ‘’ Elimu Jumuishi na usawa katika ajira ni haki ya wasioona,kwa pamoja tuondoe vikwazo ili kufikia adhima hii’’.

Kabla ya maadhimisho
hayo,kulitangulia pia maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani yanayoadhimishwa
kilele chake Septemba 30 kila mwaka na siku ya wenye mtindio wa ubongo ambao
sherehe zao hufanyika Oktoba 5 kil amwaka.
Halmashauri 2 kati ya 5 za mkoa wa
Katavi zilishiriki maadhimisho ambapo Halmshauri zilizoshiriki ni pamoja na
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda iliyopeleka wawakilishi 2 akiwemo Bw.Issack
Lucas Mlela,Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika 2 na afisa ustawi 1 huku
Halmshauri za wilaya za Mpimbwe,Nsimbo na Mlele zikishindwa kupeleka
wawakilishi kutokana na ukoesfu wa fedha.
Sherehe za siku ya walemavu
inayojumuisha walemavu wa aina zote kila mwaka ambayo hufanyika mara moja kila
mwaka inatarajiwa kuadhimishwa Desemba 3,mwa kuu.
Hata hivyo Mkoa wa Katavi kwa Ujumla umekuwa ukishindwa kupeleka wawakilishi katika maadhimisho mbalimbali kwa sababu za kukosa fedha.
Hata hivyo Mkoa wa Katavi kwa Ujumla umekuwa ukishindwa kupeleka wawakilishi katika maadhimisho mbalimbali kwa sababu za kukosa fedha.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments