BARAZA LA MADIWANI HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUFANYA KIKAO CHAKE KESHO,SHILINGI MIL.120 ZILIZOTUMIKA KINYUME NA MALENGO,BARAZA LA MADIWANI KUTOA TAMKO
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
BARAZA la madiwani Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,kesho linatarajia kufanya
kikao chake cha robo ya mwaka kwa mwaka 2016 ambapo masuala mbalimbali
yatajadiliwa ikiwemo kutoa tamko la
kubadilishwa matumizi ya Shilingi milioni 120 zilizokuwa zitumike kununulia
gari la Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo ambapo zilitumika kwa ajili ya
Masuala ya mitihani.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald) |
Katika mahojiano maalumu na mtandao
huu leo,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh.Hamad Hassan Mapengo amesema pia
kikao kinatarajia kujadili taarifa za
kamati mbalimbali za Halmshauri ili kuchanganua namna ya kutatua matatizo
yanayokwamisha maendeleo kwa wananchi.
Aidha amesema awali walipanga na
kupitisha bajeti ya kutumia shilingi milioni 150 kununua gari la mkurugenzi
ambapo kiasi cha shilingi milioni 120 zilizokuwa zimepatikana baada ya kuuza
magari mabovu na mali nyingine za Halmshauri
hiyo zikatumiwa bila baraza la madiwani kushirikishwa ambapo amesema baraza
litatoa kauli juu ya pesa hiyo haraka ili kufanikisha ununuzi wa gari la
Mkurugenzi mtendaji.
Wakati huo huo amesema,kabla ya kikao
cha kesho,leo kumefanyika vikao vya kichama ili siku ya kesho kuwepo maamuzi
katika masuala mbalimbali yanayomhusu mwananchi.
Kamati za kudumu za Halmshauri ya
Wilaya ya Mpanda ambazo zitawasilisha taarifa zake na kujadiliwa na baraza la
madiwani ni pamoja na kamati ya fedha,uongozi na mipango,taarifa ya kamati ya
elimu afya na maji,taafrifa ya kamati ya ujenzi,uchumi na mazingira sambamba na
kamati ya Ukimwi.
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments