MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AVUNJA BODI YA CHAMA WAKULIMA WA TUMBAKU MISHAMO TAMCOS
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama-Tanganyika
MKUU wa wilaya ya Tanganyika mkoani
Katavi Saleh Mbwana Mhando,ameivunja bodi ya chama cha wakulima cha tumbaku
MISHAMO TAMCOS na kuamru viongozi wote wa bodi hiyo wakamatwe haraka.
Wakulima wa Chama cha Ushirika Mishamo Tamcos katika picha wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika pichani hayupo |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akizungumza na wakulima wa chama cha Ushirika MISHAMO TAMCOS(Picha na Issack Gerald) |
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha MISHAMO TAMCOS Bw.Bw.Pridas Amakredo(picha na Issack Gerald) |
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo
kufuatia tuhuma za upotevu wa zaidi ya Shilingi milioni 140 kwa ajili
zilizokatwa kwa wakulima kwa ajili ya upandaji miti ambapo hata hivyo miti hiyo
haikupandwa.
‘’Naanza
na Yule wa kwangu,Afisa ushirika,Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda,nilimuuliza mara tatu akaniambia uongo,nilimtuma hakutekeleza,huyu
mtumishi wa umma kwenye wilaya ya Tanganyika hana nafasi,na kwa utaratibu wa
serikali ya awamu hii ya awame ya tano tunasema kwamba,mtumishi wa umma
akiharibu hahami anafia hapohapo’’alisema Mbwana Mhando.
Wakati huo huo mkuu wa Wilaya
alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda,kumsimamisha kazi
Afisa Ushirika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda kwa kushindwa
utekeleza wajibu wake na kuidanganya serikali.
MKUU wa Wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Saleh Mbwana Mhando,Septemba 15 mwaka huu wakati
akizungumza na wakulima wa chama cha msingi cha ushirika cha MISHAMO TAMCOS
aliuagiza uongozi wa bodi ya Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS na Afisa
Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda,kuhakikisha
wanalipa zaidi ya Shilingi milioni 200
zikiwemo hizo zaidi ya shilingi milioni 140 za upandaji miti ambapo wakulima
hao walidai kuwa wakulima wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya Wilaya ya
Tanganyika hawajalipwa kwa misimu 3 ya kilimo kuanzia mwaka 2011-2015 ambapo
bodi hiyo ilitakiwa ilipe kiasi hicho kabla ya Septemba 30 mwaka huu.
Miongoni mwa viongozi
wanaunda bodi ya chama hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha
Ushirika TAMCOS Bw.Pridas Amakredo.
Bodi hiyo imevunjwa
juzi
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments