MAGUFULI AWATUNUKU MAOFISA 197 WA JWTZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni
maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Sherehe hizo zimefanyika leo katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania
na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli mkoani Arusha.
Katia tukio hilo ambalo limepambwa na
magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao,limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
Kitaifa ambapo miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28 na
waliobaki wakiwa ni wanaume.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments