RAIS MAGUFULI ATAKA VIONGOZI WA DINI KUJIEPUSHA NA MIGOGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuhakikisha wanajiepusha na
migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo za
dini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati
alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes
Jackson kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine,Dkt.Magufuli amedai endapo mahali kwenye
uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazama jinsi taifa
unaloliongoza roho zake zitakavyopotea.
Misa ya kumsimika Askofu mteule Sosthenes imefanyika leo ikiongozwa
na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya.
Mbali na Rais Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi wengine
waliohudhuria ni mke wa Rais Maguli mama Janeth Mafuli,Rais mstaafu Benjamin
Mkapa.
Wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Venance
Mabeyo,Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba,Waziri wa Katiba na Sheria
Profesa Palamagamba Kabudi, Kamishna wa Uhamiaji,Dk Anna Makakala,na Waziri
Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora),George Mkuchika.
Sosthenes amesimikwa kuwa askofu kujaza nafasi iliyoachwa wazi
na Dk.Valentino Mokiwa aliyeondolewa madarakani na uongozi wa juu wa kanisa
hilo tangu mwaka jana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments