UTAPELI NJE YA IKULU NDOGO MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Taasisi
ya kupambana na kuzuia
rushwa TAKUKURU Mkoani Katavi imewakamata
watu wawili ambao walijifanya kuwa ni maafisa watasisi hiyo na kwenda kupokea
rushwa ya shilingi 400,000 karibu na majengo ya ikilu ndogo.
Watuhimiwa
hao waliofahamika kwa Majina ya Nicodemo Peter pamoja na
Peter Mwaninsawa wakazi wa Mtaa
wa Nsemlwa katika Manispaa ya Mpanda walijifanya
maafisa wa takukuru na kutapeli fedha hizo.
Tukio
hilo lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi nje ya
Ikulu ndogo ya Mkoa
wa Katavi iliyopo jirani na ofisi
ya TAKUKURU.
Mkuu
wa Takukuru mkoani Katavi John Minyenya amewaambia wandishi
wa habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia
mtego ulioandaliwa na taasisi hiyo baada
ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita
ni maafisa wa takukuru kitengo cha uchunguzi.
Alisema kabla
ya kukamatwa kwa wahumiwa hao
walimpigia simu msiri wa takukuru
na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa wa
taasisi hiyo na wanalo jalada la uchunguzi
za huhuma zinazo mkabili
msiri huyo akihusishwa na rushwa.
Hivyo
walimtaka awape kiasi cha shilingi 400,000
ili walifunge jalada hilo
kwa kufuta tuhuma zinazomkabili msiri
huyo ambaye ni afisa mtendaji
wa Kijiji cha Vikonge Wilayani
Tanganyika ambaye walidai kuwa anatuhumiwa kwa
tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa
wafugaji ambapo alikamata mifugo ya wafugaji
na kisha aliiachia baada ya kupokea rushwa ya kiasi shilingi
2,500,000.
Minyenya alieleza
msiri huyo ambaye hapendi na anapinga
vitendo vya
rushwa alilazimika kufika kwenye ofisi
ya Takukuru na kutoa taarifa juu
ya maafisa hao bandia
wa Takukuru Ndipo Takukuru
walipoanza kufanya uchunguzi juu
ya malalamiko hayo kutokana na
takukuru kutokuwa na watu wenye tabia kama hiyo
ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa
watuhumiwa.
Alisema ndipo
walipoandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao ambao
walimtaka msiri huyo awapelekee fedha hizo nje
ya jengo la Ikulu ndogo ya Katavi
kwa kuwa ni jirani
na ofisi yao
ya Takukuru ili iwe rahisi
wao kutoka ndani ya ofisi za Takukuru
na kufika kwenye eneo la tukio.
Kufuatia makubaliano hayo
ulipofika muda wa kupeleka fedha hizo
kwa maafisa hao
bandia alikwenda kuchukua fedha
zilizokuwa na namba za takukuru
na kisha kuwapelekea katika
eneo walilokuwa wamekubaliana kwa ajiri
ya kubabidhiana na mara walifika na
kupokea fedha hizo nje ya jengo
la Ikulu,ndipo walipokamatwa na Maafisa
wa Takukuru wakiwa na fedha hizo.
Minyenya amesema watuhumiwa
hao wanaendelea kushikiliwa na watafikishwa mahakamani ili
kujibu mashita mawili ya kujifanya maafisa
wa Takukuru na shitaka la pili likiwa ni ni kuomba
na kupoke rushwa.
Chanzo:Gurian wa Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments