IGP SIRO AKIWA MKOANI KATAVI AMESISITIZA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WAHARIFU NCHINI
Na.Issack Gerald
Mkuu wa Polisi nchini IGP Simon Sirro
akiwa ziarani Mkoani Katavi,amesema Jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua
kali za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uharifu mbalimbali ikiwemo
Mauaji ya watu kwa imani za kishirikina.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo
wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea ripoti ya mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuhusu hali ya ulinzi,amani
na usalama mkoani Katavi.
Aidha Siro amesema uharifu Mkoani
Katavi umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uharifu uliokuwepo katika miaka
michache iliyopita.
Wakati huo huo Kamanda Sirro ambaye
aliwasili jana Mkoani Katavi kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili,ameweka jiwe la
msingi ujenzi wa zahanati ya jeshi la polisi Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine IGP akiwa
ameambatana na maafisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi nchini pamoja na
waliopo Mkoani Katavi,amekagua na kuangalia maonesho mbalimbali ya namna jeshi
la Polisi Mkoani Katavi linavyoweza kupambana na uharifu mbalimbali.
Katika mkoa wa Katavi matukio makubwa
yaliyokuwepo miaka ya hivi karibuni ni pamoja na utekaji magari eneo la
Magorofani Wilayani Tanganyika katika barabara ya Mpanda – Kigoma.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments