WALIMU MKOANI KATAVI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UTAPELI UNAOWAANDAMA,WALIMU WASTAAFU WAPEWA MSAADA WA MABATI 120
Na.Judica
Schone-Mpanda
WALIMU
mkoani Katavi wametakiwa kuepuka kutapeliwa na watu wanaowalaghai pindi wanapopata mafao yao.
Rai
hiyo imetolewa na afisa elimu mkoa wa katavi Bw.Ernest Hinju katika hafla ya kukabidhi
zawadi ya mabati 120 yenye thamani ya sh.million 2 na laki 4 kwa walimu
wastaafu 6 kutoka halmashauri ya Mpanda
na manispaa ya Mpanda .
Aidha Bw. Hinju amewataka wastaafu hao kuendeleza
maisha waliyokuwa wakiishi wakiwa kazini na kutoiga maisha ya kigeni ambayo
baadae yataleta madhara kwao.
Kwa
upande wao walimu wastaafu wameshukuru ungozi wa chama cha walimu mkoa wa
katavi kwa moyo wa uzalendo walionao na kuahidi kuyatekeleza yote waliyowahusia
na kutodhalilisha kazi yao kwani ni muhimu sana.
Hata
hivyo katibu wa chama cha walimu mkoa wa katavi Bi Lucy Masegenya amesema chama
hicho kijimejipanga kutoa somo la ujasiliamali kwa walimu mara baada ya masaa
ya kazi kuisha ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhariri:Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments