MBUNGE MPANDA VIJIJINI:-SERIKALI INA MPANGO GANI WA KUJENGA HOSPITALI ZA WILAYA KATIKA WILAYA MPYA?
Na.Issack
Gerald
WIZARA ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) hapa nchini,imeziagiza Halmashauri zote nchini
ambazo hazina Hospitali za wilaya kutenga maeneo na kuanza kujenga kulingana na
uwezo walionao wakati serikali kuu ikiendelea na Mkakati wa kuoneza nguvu
katika ujenzi wa Hosiptali hizo.
Agizo hilo limetolewa leo bungeni Dodoma na
Naibu waziri wa Wizara hiyo Joseph Sinkamba Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa
Mpanda vijijini Mh.Suleiman Moshi Kakoso aliyetaka kujua mpango wa serikali katika
ujenzi wa Hosiptali katika wilaya hususani Mpaya ambazo hazina hosiptali hizo.
Waziri
Kandege amesema,serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imeongeza
bajeti na kufikia Zaidi ya Shilingi Bilioni 200 kutoka zaidi ya shilingi
bilioni 30 kwa mwaka wa fedha uliopita.
Mh.Kakoso
katika swali lake la nyongeza,amebainisha kuwa kukosekana kwa Hospitali za
Wilaya kwa baadhi ya wilaya hapa nchini ikiwemo Wilaya ya Tanganyika iliyopo
Mkoani Katavi kunasababisha wananchi kupata adha ya kupata huduma za kiafya.
Wilaya ya
Tanganyika ni miongoni mwa Wilaya Mpya zilizoanzishwa miaka miwili iliyopita
huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa katika sekta ya maji,afya na
miundomboinu ya barabara.
Comments