MAMBO YAMECHACHA NCHINI ZIMBABWE,JESHI LADHIBITI KITUO CHA UTANGAZAJI CHA TAIFA
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi |
Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare |
Rais Robert Mgabe akiwa na mkewe Bi.Grace Mugabe |
Hali hiyo ya wasi wasi wa
lolote imetanda nchini humo kuweza kuweza kutokea ambapo wasiwasi huo ulianza
jana jioni ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika
maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe
ZBC.
Hata hivyo
taarifa zinasema wafanyakazi wa shirika la utangazaji ZBC,wameambiwa na
wanajeshi hao wasiwe na wasiwasi kwamba uwepo wa vikosi hivyo ni kwa lengo la
kulinda eneo hilo.
Milipuko
mizito imeendelea kusikika pia huku Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha
yakionekana maeneo ya mjini Harare.
Chama tawala nchini
Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga kwa hatua yake ya
madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la
kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Marekani imesema inafuatilia
kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia
ya amani ambapo mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert
Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Naye
Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema leo
watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na hali ya sasa mjini
Harare.
Balozi wa
Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la
Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa
kufanyika kwa mapinduzi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments