MTOTO WA KAMANDA MTAAFU SULEIMAN KOVA AMEHUKUMIWA JELA MWAKA MMOJA MKOANI KATAVI KWA UTAPELI,ALIJITAMBULISHA NI MWAKILISHI WA STAR TV MKOANI KATAVI
MAHAKAMA ya mwanzo wilayani Mpanda mkoani
Katavi imemuhukumu aliyekuwa akijitambulisha kuwa ni mwakilishi wa
televisheni ya Star Tv mkoani Katavi pia mtoto wa Kamanda
mstaafu wa Jeshi la polisi Sulemani Kova anaejulikana kwa jina
la Gerald Kova mkazi wa mkoa wa Mwanza kifungo
cha mwaka mmoja jela kwa kosa la uapateli.
Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mfawidhi wa
mahakama hiyo Marko Pagyo baada ya kuridhika na ushahidi
uliotolewa na upande wa mashtaka.
Awali mwendesha mashtaka wa
jeshi la Polisi Wp Salma alidai Mahakamani hapo kuwa
mshtakiwa alitenda kosa hilo februari 8 mwaka huu
katika eneo la hotel ya Madina katika Manispaa ya Mpanda.
Alidai kuwa
mshitakiwa huyo alijipatia kwa njia ya udanganyifu
Kamera moja aina ya Canoni yenye thamani
ya shilingi 3,500,000 pia computer aina ya Laptop pamoja na stendi ya
Kamera ya video mali ya Elias Mlugala.
Alisema mtuhumiwa baada
ya kujipatia mali hizo kwa njia
ya udanganyifu alitoroka wilayani Mpanda na
kutokomea kusikojulikana.
Alisema vitu alivyotapeli ni camera aina ya
Nikon D 7,200
mali ya Chama cha Wandishi wa
habari mkoani Katavi yenye thamani ya shilingi 4,900.000.
Mwendesha mashitaka huyo
aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa
baada ya kutokomea kusikojulikana mpaka mwezi
Agosti mwaka huu alipokamatwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
akijitambulisha kwa jina la Crispin Masawe,alikamatwa
baada ya kufanya amefanya utapeli mwingine na
kujipatia Lap top moja ya mwandishi
wa habari.
Alidai baada
ya kukamatwa alifikishwa mahakama ya
mwanzo ya
Kahama na kuhukumiwa kifungo
cha miezi mitatu
au kulipa faini ya shilingi
100,000 hata hivyo hakuweza kulipa na
kwenda gerezani kutumikia kifungo.
Mwendesha mashta
alieleza ndipo waandishi wa habari wa mkoani katavi
Elias na Kibada waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo
walipopata taarifa ya kituo cha polisi cha Mpanda ya mtuhumiwa wao kuhukumiwa kifungo hicho
walianza kufuatilia.
Walifanya utaratibu na kwenda
Kahama na kumlipia faini na kumtoa gerezani
kisha akawa chini ya ulinzi wa polisi na
kusafirishwa hadi Mpanda na alipofikishwa alionesha
vifaa vyote, alivyomuuzia mfanyabiashara mmoja wa
majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi.
Mshitakiwa Gerald Kova katika utetezi
wake kabla ya kusomewa hukumu aliiomba mahakama
imwachie huru kwa kile alichodai kuwa
anakunywa dawa za kufubaza makali ya ukimwi ARVs na ana matatizo ya
ugonjwa wa sikoseli pia mama yake mzazi
ni mgonywa na anamtegemea yeye.
Baada ya utetezi
huo hakimu Paragyo
alisoma hukumu na kuamuru mshitakiwa
atumikie kifungo cha mwaka mmoja jela na pindi
atakapo toka gerezani atatakiwa kulipa shilingi
800,000.
Mshitakiwa huyo anatarajiwa kufikishwa
tena mahakamani kwa ajiri ya kesi ya pili ya kuiba kamera aina
ya Nicon mali ya Chama cha waandishi wa habari
ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Hukumu hiyo imtolewa juzi
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments