MKAZI MMOJA NSIMBO KATAVI AMEJINYONGA KWA KUTUMIA MKANDA WA SURUALI IKIELEZWA ANAKIMBIA MADENI

Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Aliyekuwa Afisa Mtendaji katika kata ya Litapunga halmashauri ya Wilaya ya nsimbo mkoani Katavi Augastino Wangabo(52) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kilichoelezwa kuwa amekimbia madeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Smith Pangani amethibitisha mtumishi wake kujinyonga akisema tukio hilo limetokea jana.
Amesema Marehemu Wangabo inasemekana alikuwa na madeni mengi pamoja na kutuhumiwa kula michango mbalimbali ikiwemo fedha ya maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru miaka ya hivi karibuni hali iliyopelekea kuondolewa katika kituo cha awali cha kazi alichokuwa amepangiwa na kurejeshwa Ofisini makao Makuu ya Halmashauri.
Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amethibitisha marehemu kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali ambapo amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha marehemu kujinyonga.
Kamanda Nyanda amesema mara baada ya marehemu kufuatwa nyumbani kwake kwa ajili ya kulipa madeni, Marehemu aliwaomba Jeshi la polisi na waliokuwa wakimdai wamsubiri kidogo aingie ndani na ndipo hakutoka nje mpaka ilipobainika kuwa amejinyonga ndani ya nyumba yake. 
Wakati huo huo kamanda Nyanda,ametoa wito kwa watu kutojinyonga kwani kufanya hivyo siyo suluhisho la matatizo bali ni kuongeza matatizo kwa waliobaki.
Hata hivyo imebainishwa kuwa awali marehemu alitajwa kumtapeli mkazi mmoja wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Nsimbo kias cha shilingi milioni 1.9 kwa ajili ya kumpatia Ajira. 

Matukio ya watu kujinyonga mkoani Katavi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo sababu za madeni,ugumu wa maisha na wivu wa kimapenzi yamekuwa yakiripotiwa. 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA