MASHA AMEJIVUA UANACHAMA CHADEMA
Aliyekuwa mwanachama CCM, ambaye baadaye alihamia Chadema,Lawrance
Masha amejivua uanachama katika chama hicho akidai upinzani wa sasa
umeridhika na hali ya kuendelea kuwa wakosoaji ili kukisaidia chama
tawala kujirekebisha.
Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
katika Serikali ya awamu nne, amesema upinzani hauwezi kutegemea kushika dola
kwa kutegemea madhaifu ya CCM badala uwezo wake kama mbadala.
Amesema kazi kubwa ya chama chochote cha siasa ni
kujiandaa na hatimaye kushinda uchaguzi ili uweze kuunda na kuendesha Serikali
na dola kama njia ya maono yaliyo kwenye ilani ya uchaguzi kwa lengo la kuleta
maendeleo na ustawi katika nchi.
Masha ambaye aliwani kuwa Mbunge wa Nyamagama mwaka 2005-10,amesema
siyo sahihi kwa vyama vya upinzani kuwekeza katika kumpinga Rais Magufuli
ambaye ni mkuu wa nchi pekee anayetekeleza kwa vitendo mambo ambayo upinzani
ilikuwa ikiyapigia kelele kwa miaka mingi,na kuwashinda viongozi wa CCM
waliomtangulia.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments