WATU WAWILI MIKONONI MWA POLISI KATAVI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO
Na.Issack Gerald-Katavi
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi ACP Damas Nyanda amesema jeshi hilo linawshikilia watu wawili wakituhumiwa
kuhamasisha maandamano kwa njia ya Mtandaoni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda |
Aidha Kamanda Nyanda ametoa onyo kali
kwa watu watakaohamasisha au kuandamana ambapo amesema watakaoandamana
watakabiliwa na hatua kali za kisheria.
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wakiwemo
Said Rashid Mdemela,Juma Bairon Mwanda,Jonathan John Midende,Paul Makelele na
Wenseslaus Obed wamesema maandamano hayo hayana tija kwa watanzania na
hawatashiriki kwa sababu ni wakati wa kufanya kazi za maendeleo na kuepuka
mkono wa sheria kwa mambo yasiyokuwa na maana.
‘’Majina ya watuhumiwa hayakuwekwa wazi kwa
sababu za kiuchunguzi na upelelezi utakapokamilika wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani’’-Alisema Kamanda Nyanda
Maandamano hayo yanayodaiwa kuratibiwa
na mwanamke Mange Kimambi aliyeko nje ya nchi,yamepangwa kufanyika Aprili 26
mwaka huu kuelekea Ikulu ya Rais kwa ajili ya kupinga baadhi ya mambo
mbalimbali yanayoendelea nchini.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments