SHIRIKA LA WATERLEED WAMETOA MSAADA WA GARI 1 NA PIKIPIKI 26 KATIKA MKOA WA KATAVI
Na.Issack
Gerald-Katavi
Shirika la Waterleeds
Program Tanzani WRP-T limetoa msaada wa gari
moja kwa Manispaa ya Mpanda na pikipiki 26 kwa
Halmashauri za mkoa wa Katavi zenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 268.
Msaada huo uliokabidhiwa jana na mkuu wa mkoa wa
Katavi Meja Gegerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa
halmashauuri zote tano za mkoa wa Katavi ni kwa
ajili ya shughuli za mradi wa kudhibiti Ukimwi
mkoani Katavi.
Akitoa taarifa ya msaada huo afisa mradi huo WRP-T
mkoani Katavi Dkt Baraka Mgiriwa amesema msaada huo
wa gari moja na pikipiki 26 umegharimu kiasi
cha shilingi milioni 268
Alisema katika msaada
huo Manispaa ya Mpanda wamepata gari moja
aina ya Picup Land Cruiser
lenye thamani ya shilingi milioni 168,987.707 pikipiki 4 aina
ya Honda, Halmashauri ya Mpanda imepata pikipiki 5, halmashauri ya
Mlele pikipiki 5, halmashauri ya Nsimbo pikipiki 6, halmashauri ya
Mpimbwe pikipiki 5 na ofisi ya Mganga Mkuu wa
Mkoa ilipata pikipiki moja zote zikiwa na thamani
ya shilingi milioni 98,800,000.
Kwaupande wake mganga mkuu wa mkoa huo wa
Katavi Dkt Yahaya Huseein alisema baada ya halmashauri
hizo kukabidhiwa misaada hiyo wana matarajio makubwa ya
kutoa huduma mbalimbali katika maeneo ya halmashauri
hizo.
Alizitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni
kuimarika kwa shughuli za usafirishaji
wa sampuli za damu kavu za watoto waliozaliwa na wakina mama
wenye maambukizi ya VVU kwa ajiri ya
kupimwa hali ya maambukizi ya watoto wao .
Pia alisema kazi nyingine ni kupunguza uharibifu wa
sampuli za damu kwa
watoto waliozaliwa na mama wenye
VVU pamoja na zile za
kupima wingi wa kiwango cha
vvu katika damu kwa
WAVIU wote kwani kabla ya msaada huo walikua
wakichelewa kusafirishwa vipimo kwenda katika maabara.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Raphael Muhuga alisema msaada huo utasaidia kuboresha utendaji
kazi kwa wagonjwa kupatiwa huduma kwa wakati tofauti na
ilivyokua hapo awali ambapo amezitaka halmashauri zote
za mkoa wa Katavi zione umuhimu
wa kuvitunza vitendea kazi hivyo na wavitumie kwa
makusudi yaliokusudiwa na si tofauti.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Mpimbwe Erasto Kiwale amesema kutoka
na jografia ya halmashauri yake, pikikpiki hizo
zitawasaidia watumishi wa afya kwenda kutoa huduma
kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa gari kwa urahisi.
Comments