MIKOA NA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO DARASA LA SABA 2017
Baraza la Mitihani la Tanzania
(Necta) limetangaza matokeo ya
mtihani wa darasa la saba huku Mkoa wa Katavi
ukiwa ni miongoni mwa mikoa kumi bora ambayo imefanya vizuri kwa kufaulisha
wanafunzi.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles
Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo
wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.
Dk
Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na
asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .
Amesema
idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.
Dk
Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo
kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.
Katibu
Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati
umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka
2016.
"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa
ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97
kulinganisha na mwaka 2016.
"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika
somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa
kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30,"
amesema Dk Msonde.
Katibu
Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo
Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga),
Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne
Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).
Amezitaja
shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga),
Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida),
Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).
Aliitaja
mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa,
Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.
Dk
Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi
na Manyara.
Comments