AJALI YA MOTO IMEUA WATU 4 USIKU WA KUAMKIA LEO
Watu wanne wamepoteza maisha usiku wa
kuamkia leo katika kijiji cha fumba wilaya ya Magharibi B Unguja kutokana na
nyumba kuteketea kwa moto mnamo majira ya saa sita na nusu usiku.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisi Hassan Nassir Ali amewataja waliofariki ni Bahati
Ali Ameir (40), Sinawema Abdalla Ali (10), Hashim Abdalla (6) na Latifa
Mohammed Ali (8).
Kamanda wa
polisi amesema tukio hilo linaaminika limesababishwa na hitilafu ya umeme
na kuwataka wananchi kuwa waangalifu katika matumizi yao ya umeme.
Comments