ROBO YA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMETUMIA SHILINGI MIL.50 KWA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI
Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,imefanikiwa kutoa mkopo shilingi milioni
hamsini kwa vikundi vya wanawake na vijana katika robo ya kwanza ya mwaka wa
fedha 2017/2018.
Hayo yamebainishwa na Afisa Maendeleo
ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bi.Halima Kitumba wakati akizungumzia kuhusu namna Halmshauri inavyotekeleza agizo la serikali kutumia
asilimia 10 ya mapato ya ndani kuwawezesha wanawake na vijana.
Katika mgao wa fedha hizo jumla ya
vikundi 8 vya wanawake ambavyo vimepata shilingi milioni 29,700,000 huku
vikundi 6 vya vijana vikipata miluioni 20,300,000.
Aidha amesema katika robo ya pili
inayoanzia mwezi Oktoba mwaka huu,wanatarajia kutumia shilingi milioni 50 kwa
vikundi 19 ambapo mpaka sasa wametoa zaidi ya shilingi milioni 11,786,000/= zilizoelekezwa
katika viwanda vidogo vidogo SIDO kwa ajili ya kununua vifaa vya uchakataji na
kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali kwa wanawake na vijana waliopo Ikola
na Isengule.
Ametaja miongoni mwa mafunzo
yaliyofundishwa ni pamoja na namna ya kuchakata samaki na daga,kutengeneza dawa
za kunguni,sabuni,batiki na vikoi,useketaji wa blanketi na masweta.
Katika mgao wa mikopo ya robo ya pili
inayoanzia mwezi Oktba jumla ya vikundi vitakavyonufaika vipo 19 ambapo katika vikundi
hivyo,vikundi 14 vya wanawake vitapata shilingi milioni 29,200,000 na vikundi 5
vya vijana vitapata shilingi milioni 11,600,000.
Kwa mjibu wa Bi.Kitumba mpaka sasa
zaidi ya vikundi 90 vya ujasiliamali katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
vinanufaika na mikopo inayolewa na Halmshauri.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments