WAKAZI MKOANI KATAVI WAMESHAULIWA KUJIUNGA NA ASASI MBALIMBALI
Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kujiunga na asasi mbalimbali za kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Emiliana Stanslaus, mkufunzi wa asasi isiyo ya
kiserikali ya Tanzania Girl Guides Association wakati wa uzinduzi wa kampeni
maalum ya You Report kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa njia ya ujumbe
mfupi.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii
Mkoani Katavi Bi Anna Shumbi amewataka
wananchi kutumia fursa hiyo ili waweze kuandaa maisha yao ya baadae kulingana
na dhima ya chama ya kuwainua kiuchumi
Tanzania Girl Guides Association imelenga kuwaendeleza wasichana na
wanawake katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments