MKOANI KATAVI DIWANI JELA MIAKA 3 KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA
Na.Issack Gerald
Mahakama ya
wilaya ya Mlele imemkumu kwenda jela diwani wa kata ya Katumba Senator Jeriti Baraka kwa kosa la kuomba na kupokea
rushwa.
Mbele ya hakimu
mkazi wa mahakama hiyo Timothy Swai, mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Bahati Haule amedai mtuhumiwa
alitenda kosa hilo 12.05.2016 kwa kuomba rushwa ya shilingi 500,000/=ili
asimuhamishe mfugaji mmoja kwenye eneo lililozuiliwa na mahakama kuendesha
shughuli za ufugaji.
Taarifa iliyotolewa
na taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa (TAKUKURU) mkoani katavi imesema mtuhumiwa amehukumiwa kwa makosa mawili
tofauti ambapo kosa la kwanza ni kuomba rushwa na kosa la pili ni kupokea
rushwa.
Taarifa hiyo
inaeleza kuwa kosa la kuomba rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kutoa faini ya shilingi
500,000/= au kifungo cha miaka mitatu na kosa la kupokea rushwa mtuhumiwa
amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela bila faini.
Katika taaifa ya Takukuru inaeleza
kuwa baada ya taarifa kupokelewa Mei 12 mwaka 2016,uchunguzi wa awali
ulifanyika kasha kuandaliwa mtego wa rushwa uliofanikisha kukamatwa kwa Bw.Senetor
Jeriti Baraka katika eneo la Msaginya Getini akipokea Shilingi 400,000/=kutoka
kwa mtoa taarifa ikiwa ni sehemu ya malipo y ashilingi 500,000/= kwani awali
alikuwa ameshapokea shilingi 100,000/=kutoka kwa mtoa taarifa kama malipo ya
awali.
Hukumu hiyo dhidi ya kiongozi huyu
aliyechaguliwa na wananchi ilitolewa Juzi Novemba 20,2017.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments