MKUU WA WILAYA YA MPANDA AINGILIA KATI MGOGORO WA TENDA YA WAJASILIAMALI KUHUSU UTENGENEZAJI WA MADAWATI.
Na.Issack Gerald-Katavi
Umoja
wa wajasiliamali Pasifiki waliopo mtaa wa majengo kata ya Kashaulili umeilalamikia Manispaa ya Mpanda kwa kutoa
tenda kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Sailoni Mwagama ambaye ni
mjasiliamali wa eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali kuwa wajasiliamali hao
wangepata tenda hiyo kwa pamoja kama ilivyokuwa imetangazwa na Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima.
Kwa
niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,akitoa ufafanuzi wa malalamiko hayo katibu
tarafa wa Tarafa ya kashauriri Bw. Reginard Muhango katika mkutano uliofanyika eneo hilo, amesema lengo na hadi ya mkuu wa
wilaya ni kutoa tenda kwa kila mwana pasifiki na si kwa mtu mmoja.
Wakati
Bw. Mhango akiwatoa wasiwasi wajasiliamali hao pia aliwaahidi kuwa huo siyo
mwisho wa tenda kufika mahali hapo.
Hata
hivyo alimuamru mwenyekiti wa eneo hilo,kugawa magogo kwa kila mjasiliamali ili
kutengeneza madawati hayo.
Aidha
ametoa wito kwa wajasiliamali hao kuendelea na kazi kama kawaida pamoja na
kudumisha umoja kati yao na kuchangamkia fursa wanazopata ili kutengeneza vitu
vyenye ubora na ustadi wa hali ya juu.
Tenda ya utengenezaji wa madawati kwa
ajili ya Shule Wilayani Mpanda ilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mnamo
Februari 27 mwaka huu ambapo zaidi ya Magogo 130 yalitakiwa kugawanywa kwa wajasiliamali
hao zaidi ya 300 badala yake kuchukuliwa na mtu mmoja hali ambayo ndiyo
imesababisha hali ya kutoelewana kwa wajasiliamali wenyewe na hatimaye
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kulalamikiwa.
Comments