CHADEMA WAPINGA TAMKO LA POLISI VIKUNDI VYA ULINZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA ,CCM WAKUBALI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimepinga kauli ya jeshi la Polisi Mkoani
hapa kupiga marufuku vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa wakati wa
kampeni na uchaguzi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama
hicho Wilayani Mpanda Abraham Mapunda wakati akihojiana na Mpanda Radio katika ofisi za chama hicho kuhusu agizo la
jeshi la polisi kutupilia mbali vikundi vya ulinzi ndani ya chama.
Akimezungumza Na Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda
Bw.Beda Katani kuhusiana na tamko la jeshi la polisi ambapo pamoja na mambo
mengine amesema anaunga mkono jeshi la Polisi kupiga marufuku vikundi vya
ulinzi ndani ya vyama vya siasa ili kuimarisha usalama.
Wakati huohuo baadhi ya wakazi Manispaa
ya Mpanda wakizungumza na Mpanda Radio mbali na kusema mengi wamelitaka jeshi
la polisi kusimamia sheria na maadili ya kazi zao katika ulinzi na kutenda haki
kwa vyama vyote vya siasa wakati wa
kampeni na Uchaguzi.
Kauli za viongozi wa vyama na maoni
ya wananchi kuhusu vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa zimekuja ikiwa ni
siku moja baada ya Mratibu mwandamizi na mnadhimu wa jeshi la polisi Mkoani
KATAVI Focus Malengo kutoa tamko hilo
kupitia Kipindi cha Polisi Jamii kilichorushwa na Mpanda Radio Alhamisi saa
kumi jioni.
Kikundi cha ulinzi cha Chadema
kinaitwa Red Briged wakati kile cha CCM kinaitwa Green guard.
Comments