SIDO KUFUNGUA OFISI ZAKE KATAVI
Na.Issack Gerald-KATAVI
Shirika la viwanda vidogovidogo SIDO
Mikoa ya Ruka na Katavi, linatarajia kuanzisha ofisi Mkoani Katavi kusogeza
huduma na kutatua changampoto mbalimbali
zinazowakabili wafanyabiashara zikiwemo mikopo na masoko
Akizungumza na P5 TANZANIA Meneja wa shirika hilo Katika mikoa ya Rukwa na Katavi Martin Chang’a
amesema kuwa wafanyabiasahara hususani wenye viwanda wanapata hasara kutokana
na kukosa mikopo na elimu ya kuongeza thamani ya bidhaa zao katika usindikaji.
Aidha ameiomba serikali ya Manispaa
ya Mpanda kutoa ushirikiano kwa shirika hilo litakapohitaji kufanyiwa hivyo.
Shirika hilo linafanya kazi Mkoani
Katavi tangu Katavi kupewa hadhi ya kuwa
Mkoa mwaka 2012
Comments