VIKUNDI VYA ULINZI VYAMA VYA SIASA VYAPIGWA MARUFUKU
Na.Issack Gerald-KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
limevitaka vyama vya siasa na wafuasi wao kuzingatia kanuni,sheria na taratibu
za vyama vyao kudumisha amani ya nchi na kuepuka makosa ya jinai yanayoweza
kuwatia hatiani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mratibu mwanadamizi
wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Focus Malengo wakati wa Mahojiano Maalum na P5
TANZANIA.
Aidha Malengo amewataka viongozi wa
vyama vya siasa,wafuasi wao na wamiliki wa vyombo vya usafiri kutotumia magari
yasiyoruhusiwa kisheria ili kuepuka uvunjifu wa sheria za barabarani na
hatimaye kuzuia ajali zisizo za lazima.
Wito huo wa jeshi la polisi unatolewa ikiwa ni
siku ya tano tangu kampeni za uchaguzi Mkuu kuzinduliwa kwa mjibu wa Katiba ya
nchi ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Comments