WANAFUNZI WAOMBA KUENDELEZWA ELIMU
Wanafunzi wakiwa darasani Shule ya msini Mpanda iliyopo Manispaa ya Mpanda |
NA.Issack Gerald-Mpanda
Wanafunzi wa shule ya msingi Mpanda iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewaomba
wazazi na walezi kuwaendeleza kielimu wanapokuwa wamehitimu masomo ya darasa la
saba na kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza.
Wanafunzi hao wakihojiana na P5
TANZANIA wamesema kuwa sababu kuwa
inayowafanya wasiendelee kielimu ni mwamko mdogo wa kielimu katika jamii.
Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw Razaro Jangu amesema
wamefanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa
kiwango cha juu.
Aidha Mwl Jangu amekiri kuwepo kwa tatizo la wazazi walio wengi kuwa
na mwamko mdogo kielimu jambo linalo kwamisha ndoto za wanafunzi hao kutokana
na wanafunzi hao kutofikia ngazi ya juu kielimu kutokana na kutelekezwa na
wazazi wao sababu kubwa ikitajwa ni umaskini na mwamko mdogo wa elimu.
Comments