CWT MPANDA YAKANUSHA KUWEPO MGOMO WA WALIMU JUMATATU AGOSTI 30
Na.Issack Gerald- MPANDA
CHAMA
cha Walimu CWT Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Kimekanusha taarifa za
Kuwepo kwa Mgomo wa Walimu siku ya Jumatatu wa Kuishinikiza serikali
kuwalipa Madai yao.
Akingumza jana na P5 TANZANIA Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda bwana Jumanne Msomba
amesema Ofisi yake haina taarifa za Mgomo huo na kuwataka walimu kusubiri tamko
la Rais wa Chama cha Walimu taifa.
Wakati taarifa za kuwepo kwa Mgomo wa walimu Wilayani Mpanda
zikikanushwa Kesho Viongozi wa Chama cha Walimu taifa
wanatarajia Kukutana na Viongozi wa Serikali ili kutafuta suluhisho la Madai
hayo.
Comments