VIJANA WATAKIWA KUTOUZA UTU WAO KATIKA MASUALA YA SIASA
VIJANA
Mkoani Katavi wametakiwa kutouza utu wao kwa kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi
yao na badala yake watathmini hatima ya maisha yao.
Wito
huo umetolewa na baadhi ya wazee wakati wakizungumza na P5 TANZANIA wamesema nguvu kazi ya mwanasiasa ni vijana hivyo kuuza
utu wao kwa mahitaji madogo wanayopewa yanaweza kugharimu maisha yao kwa kesho.
Aidha
wameaswa kuepusha chuki baina yao na kumchagua kiongozi bora atakaye fanya
mambo ya maendeleo na sio kurubuniwa kwa fedha.
Mara
kadhaa vijana wameshuhudiwa kuwa mstari wa mbele katika maandamano mbali mbali
ya wanasiasa jambo linalohatarisha maisha yao.
Comments