WAZIRI APIGA MARUFUKU MADARASA YA NYASI,TEMBE,UDONGO KATIKA SHULE ZOTE NCHINI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna
wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa
kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga
madarasa bora.
Waziri wa Tamisemi Mh.Suleiman Jafo |
Waziri
Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa
kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi
kuweza kutawala kwa ufanisi.
Waziri
Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa
Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote
yote Nchini.
Waziri
Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya
kuheshimu mipaka yao ya kazi,mahusiano kazini,kutunza Siri za Serikali na
kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Awali
akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema mafunzo haya yanakamilisha
mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa miezi nane iliyopita mpaka baada ya
mafunzo ya leo Viongozi 324 watakuwa wamefikiwa na mafunzo.
Aidha
Prof.Semboja amesema Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo
yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo
wa kufanya maamuzi wa Kimkakati kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kwa
manufaa mapana ya sasa na ya baadaye.
Akitoa
Neno la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya Mkuu wa
Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI na Taasisi ya
Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi ameahidi Umakini wa washiriki kwa
siku zote za mafunzo.
Mafunzo
haya ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa imegusa Viongozi kutoka katika Mikoa ya Mtwara,Lindi,Pwani,Tanga,Kilimanjaro
na Arusha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments