LEO NI MAADHIMISHO SIKU YA MAULIDI
Na.Issack Gerald
Waisilamu
wilayani Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wameombwa kuhudhuria maulidi ya
maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Mtume Mohamadi yanayofanyika leo.
Wito huo
umetolewa na Shehe wa baraza kuu la waisilamu Tanzania BAKWATA Wilaya ya
Mpanda Iddi Shabani Kondo Wakati
akizungumza na Mpanda Redio ambapo amewaomba waisilamu wote kudumisha amani
kataika hadhara hiyo .
Shehe
Kondo amesema kuwa Maulidi hiyo itafanyika katika kata ya Stalike halmashauri
ya nsimbo kuanzia saa 1:30 jioni.
Amesema
katika kuadhimisha siku hiyo waisilamu wote wanakumbuka kazi iliyofanywa na
mtume Mohamadi ya kufikisha ujumbe rasmi wa mafundisho wa uisilamu.
Maulidi
hii ya mwaka 1439 wa dini ya kiisilamu sawa na mwaka 2017 kitaifa yatasomwa
wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na tarehe 1/12 itakuwa ndio siku ya mapumziko.
Habari
Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED
Comments