WAKAZI MPANDA WANAISHI KWA HOFU YA USALAMA, WASHINDWA KUFANYA KAZI
Na.Issack
Gerald
Wakazi wa vijiji vya Ndui
Stesheni,Mnyaki A na Mnyaki B kata ya Katumba wilayani Mpanda Mkoani Katavi wanashindwa kufanya kazi za maendeleo kwa uhuru
kutokana na uharifu unaofanywa na watu wasiojulikana.
Hali hiyo
imebainishwa na wakazi wa vijiji hivyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kwa
Nyakati tofauti katika vijiji hivyo kutokana na matukio ya watu kuvamiwa
nyumbani nyakati za usiku,kutekwa njiani na kuporwa mali.
Wakazi wameliomba jeshi la polisi
kuweka mkazo ili kutafuta namna ya kukomesha uharifu huo ambao umekuwa kero
kwao.
Mmoja wa viongozi katika maeneo hayo
Bw.Hussein Nasri ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni,amekiri
kuwepo kwa matukio ya kiuharifu hasa unyang’anyi wa pikipiki matukio ambayo
hivi karibuni yameripotiwa na wenyeviti wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B.
Hivi karibuni,Kamanda wa Polisi
Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda,akihojiwa na Mpanda Radio,alitoa kauli kuwa
hajapokea za taarifa za kiuharifu za hivi karibuni hali ambayo imeibu maswali mengi
miongoni mwa raia kuhusu mawasiliano kati ya kituo cha polisi Katumba na Makao
makuu ya Polisi Mkoa.
Habari
Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED
Comments