WAZIRI WA MAJI NAYE AMTUMBUA MHANDISI WA MAJI MKOANI RUKWA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
amemsimamisha kazi Mhandisi Goyagoya Mbena kwa tuhuma za kusaini barua ya
kuruhusu ujenzi wa mradi wa Maji wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Taarifa ambayo imetolewa jana na Wizara
hiyo,imeeleza kuwa Mhandisi Mbena amesaini barua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
wizara hiyo kinyume cha utaratibu.
Mradi huo wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa umeelezwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7.4.
Mradi huo wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa umeelezwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7.4.
Siku ya Juzi
Waziri wan chi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mh.Suleiman
Jafo,alimsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi
Mkoani Rukwa Julius Kawondo kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa na matumizi
mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni.
Chanzo:eatv
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments