TAAS MKOANI KATAVI WAMEKATAA KUITWA WALEMAVU WA NGOZI
Na.Issack Gerald
Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS)
Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye ulemavu wa
ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino.
Mwenyekiti wa TAAS Mkoani Katavi Victus Kweka |
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama
hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga
ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za watu wenye ulemavu kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu,afya na haki
nyingine za kibinadamu.
Amesema
rangi ya ngozi waliyonayo watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao
wanahesabika katika kundi la watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali
waliyonayo.
Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa.
Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa.
Amewataka
watu wenye ualbino kuchanganyikana na jamii ili kupata elimu inayowawezesha
kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya kupunguza mionzi mikali ya jua.
Watu wenye
ualbino Tanzania wamekuwa hawachangamani na jamii wakiogopa mauaji dhidi yao
kama ilivyokuwa katika miaka michache iliyopita.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments