THAMINI UHAI WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA MKONI KIGOMA
Shirika
la Thamini uhai limejitolea dawa na vifaa tiba takribani aina 50 katika vituo
vya afya 46 ndani ya mkoani Kigoma huu vyenye thamani ya shiling million 127 lengo
likiwa ni kusaidia vituo hivyo kutoa huduma stahiki na kupunguza vifo kwa akina
mama wajawazito na watoto wachanga.
Akizungumza
katika makabidhiano ya vifaa hivyo daktari Bingwa wa magonjwa ya akina mama ya
uzazi kutoka shirika hilo Dkt.Sande Dominick amewataka watoa huduma kutumia
dawa na vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwa.
Kwa
miaka kadhaa sasa idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya
imeongezeka kutoka asilimia 38 hadi kufikia asilimia 60 yote ni kutokana na
jitihada za mashirika binafsi ambapo Meneja mahusiano na mawasiliano kutoka shirika
la thamini uhai Viktoria Marijani amesema wamekuwa wakifanya hivyo ili kuokoa
maisha ya mama na mtoto.
Akimwakilisha
Kaimu katibu tawala Mkoani Kigoma mhandisi Aziz Mtabuzi,Dkt
Lameck Mdengo ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake baada ya kupokea
msaada huo ametoa shukrani Kwa niaba ya serikali na kutoa rai kwa vituo vya
afya vyote 46 kutumia msaada huo kama ilivyotarajiwa.
Hata
hivyo bado serikali inaalika wafadhili wengi kufika na kufadhili shughuli za miradii
ili kuhakikisha huduma za afya zinakuwa endelevu mkoani Kigoma lakini pia kupanua wigo wa kufadhili
katika mkioa mingine ya Tanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments