JSI WARUDIA KUFANYA TENA MKOANI KATAVI
Manispaa Ya
Mpanda mkoani Katavi imesema itaendelea
kushirikiana na Shirika la JSI la Marekani linalojihusisha na masuala ya jamii
katika kudhibiti mambo yanayomkatisha mtoto kutimiza ndoto zake.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu Meya manispaa ya Mpanda Oswadi Rwezana wakati akikabidhi
baiskeli 15 na kabati zilizotolewa na
shirika hilo JSI kwa wasimamizi wa
mashauri ya watoto ngazi ya jamii kutoka kata 15 za manispaa ya Mpanda
Naye
mratibu wa mafunzo na msimamizi wa JSI Clarence Mkoba amesema kupitia shirika hilo limeazimia kushirikiana
na wizara ya afya katika kukamilisha mradi huo kwa halmashauri 84 ikiwemo ya
Mpanda
Selestin
Antony Muhenga na kutoka kata ya kasokola na Frola Bruno Mwasala Kutoka kata ya
kazima ni Miongoni mwa watoa huduma ngazi ya jamii waliopatiwa Vifaa hivyo
wamebainisha kutasaidia kuwafikia walengwa.
Januari 12 mwaka huu,shirika la JSI
lilitoa msaada wa baiskeli 5 kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya
jamii wa Manispaa ya Mpanda.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments