RAIS MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE WA PAUL KAGAME AAGANA NA BALOZI WA ZIMBABWE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli jana amekutana
na Mjumbe Maalum wa Rais wa Rwanda na aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Dkt.Donald Kaberuka na kuzungumzia masuala mbalimbali
yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU).
Baada
ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa Dkt.Kaberuka amesema uchumi wa
Tanzania unakua vizuri na amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia
ukuaji wa uchumi huo.
Dkt.Kaberuka
amesema katika mazungumzo hayo pia amewasilisha ujumbe wa Rais wa Rwanda Mhe.Paul
Kagame ambaye kuanzia mwezi huu atakua Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na
ndiye aliyekabidhiwa majukumu ya kufanya mabadiliko ndani ya umoja huo.
Wakati
huo huo,Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini
anayemaliza muda wake Mhe. Edzai Chimonyo na kumpongeza kwa uwakilishi mzuri
alioufanya kwa miaka 10 aliyoiwakilisha Zimbabwe hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa,Mhe.Rais
Magufuli amemuomba Mhe.Chimonyo kumfikishia salamu za pongezi Mhe.Emmerson
Mnangagwa kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zimbabwe na amemuhakikishia kuwa
Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri wa kihistoria na kidugu
uliopo kati yake na Zimbabwe.
Mhe
Chimonyo ameshukuru kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chake cha
Ubalozi hapa nchini na amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa namna anavyoiongoza
nchi huku akitaja baadhi ya mambo yanayofanywa kwa mafanikio makubwa kuwa ni
mapambano dhidi ya rushwa,ujenzi wa miundombinu hususani barabara,madaraja na
viwanja vya ndege.
Mhe.Chimonyo
ambaye alikuwa kiongozi wa Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini na Kaimu Kiongozi wa Mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania
amesema Mabalozi hao wanafurahishwa na wanaunga mkono juhudi mbalimbali
zinazofanywa na Mhe.Rais Magufuli ikiwemo kuhamia makao makuu Dodoma.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments